Baada ya ziara ya mkuu wa mkoa Dar es salaam, Paul Makonda kwa siku kumi kusikiliza kero za Wananchi pamoja na kuzitafutia ufumbuzi, amesema aligundua moja ya matizo linalowasumbua wengi ni uelewa mdogo wa Wananchi kuhusu sheria na imepelekea kupoteza haki na ucheleweshaji wa kesi Mahakamani.
RC Makonda amesema licha ya wadau wa kisheria mkoa wa Dar es salaam, Wananchi wengi wameshindwa kufikiwa kwa wakati kiasi cha kusababisha kuhangaika zaidi kwa kutafuta huduma ya msaada wa kisheria.
Kutokana na umuhimu wa huduma hiyo ameona ni vyema wakapatikana vijana ambao ni Wataalamu wa sheria ili wawasaidie Wananchi wa Dar es salaam na ndio maana ameamua kuja na mkakati wa vijana Wanasheria 35 ambao watatoa huduma ya msaada wa sheria bure kwenye wilaya zote za mkoa wa Dar es salaam.
Tazama hii video hapa chini itakukutanisha na vyote alivyosema Makonda
VIDEO: Mpango mpya wa RC Makonda kwa Wamachinga Dar es salaam, Bonyeza play hapa chini kutazama