Amplifaya Top10

Stori 10 za AMPLIFAYA March 20 2014, kuhusu shabiki wa Yanga aliefariki na mengine.

on

top 10 1Amplifaya ni show ambayo inasikika kupitia Clouds FM Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa moja usiku ikihusika kutoa stori zote kumi kubwa za siku za siasa, muziki, michezo, movies, maisha na ishu nyingine.

#AMPLIFAYA March20 #10 ANC: Rais Zuma hatojiuzulu sababu ya kashfa ya kutumia pesa za umma kujenga makazi yake ikiwemo nyumba 4 za wake zake.

#9 Waziri mkuu Australia athibitisha vitu kama mabaki ya ndege kuonekana baharini, hali ya hewa imekwamisha kuvifikia, inasadikiwa huenda vikawa vya ndege ya Malaysia iliyopotea zaidi ya siku 10 zilizopita.

#8 Mgombea Ubunge Chalinze Ridhiwani kikwete amekiri kuona matatizo ya wafugaji na wakulima, kaahidi kuweka mpango bora.

#7 Kitengo cha mabomu Kenya kimelipua kilo 173 za vilipuzi vilivyokamatwa baada ya jaribio la kigaidi kufeli Mombasa.

#6 Tanzania @50 #kuwaMzalendo Afande Sele anasema inawezekana asingekua msanii leo kama sio muuza mitumba Ramadhan Mataka.

#5 Yanga & Simba zimeagizwa kulipa milioni 25 kama faini kutokana na uharibifu wa viti ktk vurugu zilizofanywa na mashabiki Yanga vs Al Ahly

#4 Rais Mugabe apunguza mishahara ya Wakuu wa mashirika ya Umma, kipato cha mwezi cha wastani kwa Wahudumu ni zaidi ya laki5 za Tanzania.

#3 Saudi Arabia imepiga marufuku Wazazi kuwaita watoto wao kuanzia sasa majina 50 yaliyo kinyume na tamaduni na dini yakiwemo Rama, Alice na Binyamin.

#2 Dogo Janja ‘Nawaomba msamaha mashabiki na Tiptop Connection yenyewe, sasa niko tayari kurudi Tiptop.. tusahau ya kale’

#1 Daktari asema >> ‘Mke wa shabiki wa Yanga aliefariki uwanjani kwenye mechi ya Yanga vs Azam asema mume wake huyu mwenye umri wa miaka 48 aliishiwa nguvu muda mfupi tu baada ya kuinuka na kushangilia goli la Yanga, baada ya hapo alikaa alafu akamlalia, muda mfupi baadae ikathibitishwa amefariki’

Ili kuwa karibu zaidi na kila stori inayotoka iwe usiku au mchana unaweza kujiunga na mtu wako wa nguvu kwenye twitter.com/millardayo facebook na instagram.com/millardayo

Tupia Comments