Michezo

Simba SC wamemalizana na Mbeya City, Ubingwa wanautaka

on

Simba SC bado wanaendelea kuonesha dhamira ya kutetea taji lao la Ligi Kuu Tanzania bara msimu huu, kwani leo wakiwa katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City wamezichukua point zote tatu licha ya uwepo wa ushindani mkubwa baina ya timu hizo mbili.

Uwanja wa Sokoine katika miaka ya hivi karibuni Simba amekuwa akikutana na wakati mgumu lakini amefanikiwa kupata ushindi wa magoli 2-1 licha ya Mbeya City kuanza kupata goli la mapema kupitia kwa Iddy Naldo dakika ya 22 ila Jonas Mkude aliisawazishia Simba SC dakika ya 68.

Meddie Kagere akadhihirisha ubora wake tena kwa kufunga goli la ushindi la Simba dakika ya 84 wakati ambao wengi walikuwa wanaamini game hiyo itaisha kwa sare ya 1-1, Simba SC wanaendelea kuwa nafasi ya pili kwakuwa na point 75 wakiwa wamebakiza michezo 9 wakati Yanga wanaongoza kwa point 80 wakiwa na michezo minne imesalia, Mbeya City wao wapo nafasi ya 11 wakiwa na point 40.

Kigezo kilichoichuja Yanga na kuipa Simba SC nafasi ya kucheza na Sevilla ya Hispania

Soma na hizi

Tupia Comments