Michezo

John Bocco azichanganya Polokwane na Simba, Polokwane watoa ushahidi

on

Ni siku moja imepita toka uongozi wa Simba SC utangaze kuwa umemuongezea mkataba wa miaka miwili nahodha wao John Bocco ambaye mkataba wake ulikuwa unamalizika, baada ya kutangazwa kuwa amesaini club ya Polokwane FC ya Afrika Kusini imeibuka na kusema kuwa Bocco ni mchezaji wao.

Inadaiwa kuwa John Bocco ambaye mkataba wake na Simba SC ulikuwa unamalizika June 31, ameingia mkataba wa miaka miwili wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi ila kwa mujibu ya picha zinazoendelea mitandaoni ni kuwa Bocco alitakiwa kutambulishwa na Polokwane July 1.

Club ya Polokwane City ni miongoni mwa club 16 zinazoshiriki Ligi Kuu ya Afrika Kusini na msimu uliomalizika wa 2018/2019 ilimaliza ikiwa nafasi ya tano katika msimamo, hivyo haijulikani kipi ndio hatma ya John Bocco baada ya kudaiwa kusaini timu mbili.

EXCLUSIVE: Msuva kuhusu kitendo cha Salamba kuomba viatu vya Banega

Soma na hizi

Tupia Comments