Michezo

Hawa ndio wachezaji wa Simba SC waliotajwa kuikosa Azam FC

on

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu soka Tanzania bara Wekundu Wa Msimbazi Simba leo asubuhi walikamilisha maandalizi ya mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Azam FC, kwenye viwanja vya Gymkhana jijini Dar es salaam.

Mabingwa hao wa Tanzania bara mara mbili mfululizo kesho watashuka Uwanja mkuu wa taifa jijini Dar es Salaam, huku wakichagizwa na mwendelezo wa kumbukumbu nzuri ya ushindi walioupata katika michezo minne ya Ligi Kuu msimu huu, ambao umewafanya kuwa kileleni mpaka dakika hii.

Kocha mkuu wa Wekundu hao wa Msimbazi Patrick Aussems amesema kikosi chake kipo tayari kwa mpambano huo wa kesho na ana matarajio makubwa, kocha Aussems amethibitisha kumkosa beki wa pembeni na nahodha msaidizi Mohamed Hussein Tshabalala, kiungo Jonas Mkude pamoja na Shomari Kapombe ambao ni mejeruhi.

AUDIO: SERGIO AGUERO WA MAN CITY AMEPATA AJALI

Soma na hizi

Tupia Comments