Kocha wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger ameweka wazi kwa nini hakufundisha timu yoyote England baada ya kuachana na Arsenal, Wenger baada ya kuachishwa kazi alieleza kuwa alipokea ofa zaidi ya mbili ya kuzifundisha club za England lakini alikataa.
Wenger leo ameweka wazi kuwa sababu kuu ya kuzikataa ofa hizo kwani angekuwa anaona kama anajihusisha na Arsenal japo sio moja kwa moja, Wenger hadi anaachishwa kazi May 2018 alikuwa ameifundisha Arsenal kwa miaka takribani 22.
“Mimi ni Arsenal na baada ya hapo mimi mwenye weledi, niliamua kuondoka nje ya Ligi Kuu ya England kwa sababu ingekuwa inanihusisha sana na Arsenal, nilipata fursa za kurudi kufundisha England lakini nimezipiga chini, sitaki kukwambia ni club gani kwa sababu kuna watu wanazifundisha itakuwa sio fair kwao”>>>Wenger
Msimu uliopita Wenger alikuwa akihusishwa kujiunga na Fullham na AC Milan ya Italia, ila kwa sasa amefungua milango ya kurudi uwanjani kufundisha soka kwa mara nyingine tena lakini anahusishwa pia kuwa anaweza kwenda kuwa mtu wa ufundi wa FIFA.
VIDEO: Goli lililoipa Tanzania Ubingwa wa CECAFA U-20 dhidi ya Kenya