Makamu wa Rais wa Startimes Carter ametoa shukrani zake za dhati kwa mwakilishi wa Waziri Mkuu Bi.Jenista Muhagama na TACAIDS katika Maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika jijini Mwanza kwa kuipa tuzo StarTimes na kusema kwamba itajitahidi kwa kadri ya uwezo wake kuchangia na kuisaidia Serikali kupambana na vita dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Startimes imepata tuzo hiyo kupitia kipindi cha Bongo Star Search na imelenga Kusaidia na kuelimisha vijana juu ya maambukizi ya VVU ambao vijana ndio walengwa wakubwa.
Katika maadhimisho hayo Carter alitoa mchango wa Tsh Millioni 5 kuchangia mapambano dhidi ya Ugonjwa wa UKIMWI.