Mix

Majibu ya Jeshi la Polisi Makao Makuu kuhusu tuhuma za Rushwa dhidi ya Sirro

on

Baada ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kudai mbele ya Waziri Mkuu kuwa Wafanyabiashara wa Shisha walitaka kumhonga ili asiliongelee suala hilo lakini bado biashara hiyo ikaendelea na kumfanya ahisi kuwa Kamanda Sirro amepokea rushwa na kuwaruhusu waendelee kufanya biashara ya Shisha.

Leo November 18, 2016 Jeshi la Polisi Makao Makuu kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Robert Boaz ametoa taarifa juu ya suala hilo. Kaimu DCI Robert amesema kuwa wamelipokea suala hilo na wameviachia vyombo husika vinavyohusika na masuala ya rushwa.

“Jeshi la Polisi limepokea taarifa za tuhuma hizo na kwa mujibu wa taratibu za Jeshi la Polisi inapotokea kiongozi yeyote wa Jeshi hilo amepatwa na tuhuma ni lazima achunguzwe ili kubaini ukweli, Jeshi la Polisi tayari limeanza uchunguzi juu ya tuhuma hizo.”- Kaimu DCI Boaz

VIDEO: Ipo hapa taarifa ya Jeshi la Polisi kuhusu watu ambao hawajasalimisha silaha zao mpaka sasa na maamuzi ya mapya

Soma na hizi

Tupia Comments