Waswahili husema ‘Kutoa ni Moyo si utajiri’ wakiwataka watu kutoa sehemu ya walichojaaliwa na Mungu kwa watu wengine wenye uhitaji msemo ambao umemgusa pia Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula ambaye ameamua kuutumia Mwezi huu Mtukufu wa Ramadhan kutoa sehemu ya alichojaaliwa.
Mabula ambaye yupo Jimboni kwake kwa shughuli za maendeleo ya Jimbo hilo ameziambia Ayo TV na millardayo.com kuwa ametoa sehemu ya alichojaaliwa kuchangia ukarabati wa Msikiti wa Mahina kwa kutoa baadhi ya vifaa vitakavyotumika kwenye ukarabati huo.
Kitu Waziri Mwigulu amewaambia Watanzania kuhusu JPM, makinikia!!!