Habari za Mastaa

Man Water aongelea WASAFI kutoa ngoma baada ya Alikiba

on

August 25, 2017 mwimbaji staa wa Bongofleva Alikiba aliachia video ya wimbo wake mpya unaoitwa ‘Seduce Me’ ambao umekuwa gumzo ambapo saa chache baadaye WCB wakiongozwa na Diamond Platnumz waliachia video yao mpya pia ‘Zilipendwa’ kitendo kilichopokelewa kwa hisia tofauti.

Mmoja wa watu waliopokea tofauti ni pamoja na Producer wa ‘Seduce Me’ Man Water ambaye amekaa na Ayo TV na millardayo.com ambapo pamoja na mambo mengine imezungumzia ishu hiyo akisema lazima wasanii wanapoachia nyimbo zao lazima wapeane nafasi na kama wimbo uliotoka baada ya Alikiba basi hautadumu kwenye soko, utapotea.

>>>”Wasanii ufike wakati tusifanye kwa ushindani… kama upande mmoja umeshaachia wapeane nafasi kama tunataka kujenga na kutengeneza hits vinginevyo tusipoangalia tutaua, tunaziua na wasanii watapotea kwa haraka sana kwa sababu hazitokuwa kazi za ubunifu bali za kupanic’

“Kama kuna ngoma imetoka katika hali ya ushindani, nina uhakika kwamba asilimia kubwa itapotea. Siitabirii vibaya ila kuna mambo ya kujipanga ili kupeana nafasi.” – Man Water.

STATUS ZA HIZI VIDEO 2 MPYA: Seduce me na Zilipendwa

Esma Platnumz kaingilia kati baada ya Dimpoz kupost picha ya Mama Diamond

HAUTAKI KUPITWA??? Kuna hii APP MPYA YA MILLARD AYO kwa wewe wa ANDROID unaweza kubonyeza hapa moja kwa moja kwenda kui-download mtu wangu, HABARI ZOTE KIGANJANI MWAKO >>> APP MPYA BONYEZA HAPA

Soma na hizi

Tupia Comments