Habari za Mastaa

Spidi ya gari yamgharimu Quick Rocka

on

Mkali wa Rap nchini Quick Rocka ametumia ukurasa wake wa instagram kuelezea kuhusiana na gari lake kuharibika engine hii ni baada ya kujaribu kuendesha umbali wa kilomita 250 kwa saa moja.

Quick Rocka ametoa onyo kwa watu na kusema kuwa asingependa kumuona mtu akijaribu kufanya hivyo kwasababu wataishia kununua engine mpya na kibaya zaidi mtu anaweza kuishia kwenye jeneza kutokana na kuonekana ni hatari kuendesha kwa spidi hiyo.

“Nimejaribu kilomita 250 kwa saa na nikaishia kuharibu engine  yangu, endelea kusubiri mpenzi baba atakununulia engine nyingine mpya *ONYO* Usijaribu kufanya hivi utaishia kununua engine mpya au kibaya zaidi utaishia kuwa kwenye jeneza”

RADO: Rais akilala, akiamka ni muda wa BONGO MOVIE’

Soma na hizi

Tupia Comments