Baada ya kuwa na wakati mgumu msimu uliopita kwa shirikisho la soka Tanzania TFF kutokana na Ligi Kuu kukosa mdhani kwa msimu mzima, msimu huu umekuwa na neema kwa TFF kupata mfululizo wa wadhamini katika mashindano mbalimbali.
TFF baada ya kusaini mkataba na Azam Media wa miaka 4 wenye thamani ya Tsh Bilioni 4.5 kwa ajili ya kuonesha Kombe la FA, huku wakuonesha mechi za Taifa Stars za kirafiki ukiwa ni mkataba wa Tsh milioni 400 sawa na Tsh milioni 100 kwa kila mwaka, Rais wa TFF Wallace Karia kaomba vyombo vya habari kutoa mileage kwa wadhamini ili kuwavutia zaidi.
EXCLUSIVE: SAMATTA KAFUNGUKA DILI LAKE KWENDA ENGLAND, VIPI CHAMPIONS LEAGUE