Michezo

PICHA 3: Zitto Kabwe amemtembelea Samatta Ubelgiji

on

Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe leo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii amewajulisha watanzania kuwa amefanikiwa kufika nyumbani kwa nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta.

Zitto amefika nyumbani kwa Samatta nchini Ubelgiji katika mji wa Genk na kumjulia hali na amethibitisha kuwa Samatta anaendelea vizuri.

“Jana jioni nilikwenda Genk, hapa Ubelgiji, nyumbani kwa Nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, ndugu Mbwana Ally Samatta, ambaye ni mchezaji wa Klabu ya KRC GENK inayoshiriki Ligi Kuu ya hapa Ubelgiji”>>>Zitto

“Inatia moyo zaidi kuona Kijana huyu mwenzetu wa Kitanzania namna anavyofanya kazi kwa bidii ili aweze kufanikiwa zaidi, namuomba Mola amuwezeshe kutimiza ndoto zake”>>>Zitto

VIDEO:Magoli ya Simba walivyorudi kimataifa leo vs Gendermarie Full Time 4-0

Soma na hizi

Tupia Comments