Jeshi la Polisi Tanzania limechukua headlines kwa siku za hivi karibuni kwa kudhibiti uhalifu katika sehemu mbalimbali za nchi. Leo March 3 2016 Kamishina wa Polisi wa Oparesheni na Mafunzo, Nsato Marijani amezungumzia mikakati zaidi katika kupambana na wauza Dawa za kulevya na wafanyabiashara wa bidhaa za magendo.
Kamishina Marijani amesema….>>>‘tutafilisi mali zao zinazotokana na biashara haramu ya dawa za kulevya na tutawafutilia kokote watakapokimbilia, tutawakamata na kuwarudisha nchini kujibu mashtaka’
Marijani pia aliwaonya wanaotumia bandari Bubu kukwepa kodi kwa biashara za magendo ….>>> ‘tunajiimarisha kidoria tukishirikiana na wenzetu wa mamlaka ya kodi ya mapato katika kudhibiti magendo katika bandari bubu za pwani ya bahari ya hindi na maziwa yetu‘
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na MillardAyo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE