Habari za Mastaa

Baada ya Kulazwa kwa siku Nne, ipokee taarifa hii kumhusu Rick Ross

on

Leo March 6, 2018 nakusogezea stori kumhusu Rapper Rick Ross ambae jana nilikuletea taarifa kuwa kalazwa kwa ugonjwa ambao haukuwekwa wazi. Hatimaye ameruhusiwa baada ya kuwa chini ya uangalizi wa madaktari kwa siku 4 ambapo Siku ya Jumamosi iliyopita alipata shida ya kiafya, baada ya kupoteza fahamu na kushindwa kupumua.

Taarifa zinadai kuwa Rapa huyo ameruhusiwa kwenda nyumbani baada ya hali yake  kuwa sawa huku kupitia ukurasa wake wa Instagram siku ya jana March 5, 2018 alipost picha ya mkono wake ukiwa na saa za thamani nakuweka caption ya FloridaBoy ikiwa ni eneo ambalo star huyo alizaliwa.

YOUNG D: “Sijaona hasara kufungiwa Bongo Bahati mbaya”

Soma na hizi

Tupia Comments