Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amemtuhumu Msajili wa Vyama vya Siasa akidai anaihujumu CUF kwa kutumia Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA).
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo June 28, 2017 Maalim Seif amesema Chama hicho kina taarifa kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA ameshinikizwa kuandisha wajumbe feki wa Bodi ya CUF.
>>>”Mbinu chafu iliyopangwa kufanywa na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini, yaani RITA kwa maelekezo ya Dola kupitia Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi kwa lengo la kumnusuru kibara wao Ibrahim Harouna Lipumba kwa kuhakikisha kwamba Wajumbe wa Bodi ya Udhamini fake waliopelekwa na kibaraka Lipumba wanasajiliwa baada ya kuona Bodi halali ya CUF ni kikwazo katika kufanikisha mipango yao haramu.” – Maalim Seif.
Hii VIDEO ina kila kitu…bonyeza PLAY kutazama!!!
FULL VIDEO: MC Pilipili na Eric Omondi walivyochekesha DSM!!!