Mix

Pesa atakayolipwa atae mtaja alielipua mabomu Arusha.

on

Screen Shot 2014-04-16 at 1.50.25 PMBomu la kienyeji lililolipuka ‘Arusha night park’ April 13 2014 Mianzini Arusha na kujeruhi watu 17 waliopelekwa kwenye hospitali tatu tofauti limefanya dau lililotolewa na Polisi liwe kubwa zaidi kwa yeyote atakaefichua muhusika wa huu mtandao wa mabomu Arusha.

Kamishna wa makosa ya jinai (DCI) Isaya Mghulu  amesema watatoa shilingi milioni 10 kwa huyo atakaefanya kweli kwenye kufanikisha Walipuaji mabomu hao kujulikana na kukamatwa.

Screen Shot 2014-04-16 at 2.06.01 PMKwenye sentensi nyingine, ameweka wazi kwamba mpaka sasa bado hata wale waliohusika na ulipuaji wa mabomu kwenye kanisa kule Olasiti na kwenye mkutano wa CHADEMA hawajakamatwa wala kujulikana lakini jitihada za kuwatafuta zinaendelea.

Pata kila kinachonifikia iwe usiku au mchana, nitakutumia kwenye twitter instagram na facebook @millardayo

Tupia Comments