Habari za Mastaa

Unaambiwa katika matukio yote ya Akon hili la kumtupa mtu hawezi kulisahau

on

Screen Shot 2014-04-29 at 1.32.14 AMAkon ni miongoni mwa mastaa wa muziki ambao waliteka sana chati za muziki duniani kati ya miaka ya 2003 mpaka 2008 kwa single kama lonely, right now, smack that, beautiful na nyinginezo.

Ustaa wake ulimfanya atembee sehemu mbalimbali kufanya showz ambazo baadhi yake zilichukua headlines kutokana na alichofanya kwa mashabiki ikiwemo hili tukio la kumrusha shabiki kutoka kwenye stage.

Ilikua hivi: Shabiki mmoja mzungu alimrushia kitu kwenye stage wakati Akon akiendelea na show, ni kitendo ambacho kilimkasirisha sana japo hakuonyesha mabadiliko sana kwenye sura yake lakini kiukweli kilimpa hasira na kujiuliza huyu mwenye ngozi nyeupe alimdharau kiasi gani.

Alichofanya Akon ni kumuita kwa lugha ya kikarimu yule shabiki kwenye stage na alipomfikia alimnyanyua na kumtupa chini walikokua wamesimama mashabiki wengine ambapo shabiki na mashabiki wengine waliumia kichwa, shingo na sehemu nyingine za mwili.

Unaweza kutazama jinsi ilivyokua hapa kwenye hizi video chini

Hata hivyo Akon anakiri kwamba unapokua staa kuna wakati unajisahau kwamba wewe ni mtu maarufu na kila unachofanya kinaangaliwa hivyo ni somo la kujifunza ndio maana hawalaumu sana kina Justine Bieber na Chris Brown.

Kuna makosa kama kupiga Mwanamke au kosa jingine lolote ambalo akilifanya mtu wa kawaida halitakua kubwa sana ila akilifanya mtu maarufu ndio litamulikwa mpaka basi.

Tupia Comments