Michezo

Mwanasiasa wa Tanzania aliemsupport Dani Alves kwa kula ndizi

on

Screen Shot 2014-04-30 at 5.12.47 PMKwenye mechi kati ya Barcelona na Villareal kuna shabiki mmoja alimrushia ndizi Mbrazil Dani Alves anaeichezea Barca kitendo ambacho kilionyesha kabisa ni ubaguzi wa kufananishwa na Nyani ambapo Dani aliiokota ndizi hiyo na kuila kabla ya kupiga mpira wa kona na kuifanya kama sio ishu.

Baada ya hapo Dani alisema aliamua kula ndizi hiyo kwa sababu baba yake mzazi aliwahi kumwambia kuhusu umuhimu wa mwili wa mwanadamu kupata ndizi.
Screen Shot 2014-04-30 at 5.09.25 PMNi kitendo kilichosifiwa sana na baadae kuwa topic kubwa ambapo mastaa mbalimbali wamejitokeza kumsupport Dani na kupinga ubaguzi kwa kupiga picha wakiwa wanakula ndizi ambapo miongoni mwao ni Staa wa muziki kutoka Nigeria Davido, mastaa wa soka kama Emmanuel Adebayor, Samuel Eto’o, Neymar na wengine.

Support inaendelea ambapo time hii ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe katuma picha zake na yeye.

Screen Shot 2014-04-30 at 10.08.23 AM

Tupia Comments