Wizara ya mambo ya Nje Tanzania imesema Mtanzania Nemes Tarimo alifariki akiwa vitani nchini Ukraini baada ya kujiunga na kikundi cha kijeshi kinachofamika kama Wagina akiwa anatumikia sehemu ya kifungo chake cha miaka saba alichofungwa kwa makosa ya kiharifu.
Waziri wa Mambo ya nje wa Tanzania Dkt Stergomena Tax amesema “Tarimo akiwa gerezani alipewa nafasi ya kujiunga na kikundi cha kijeshi Wagina kwa ahadi ya kulipwa fedha lakini kwa ahadi ya kuachiwa huru mala baada ya Vita na umauti ulimkuta tarehe 24 oktoba mwaka jana na wizara inawasiliana na serikali ya urusi na kuiabidhiwa kwa familia na mwili umeondoka urusi asubuhi ya leo.