Amplifaya Top10

Habari 10 za Amplifaya May 9 2014, Edinson Cavani, katibu mkuu chama kipya cha siasa

on

Screen Shot 2014-05-09 at 9.20.13 PMAmplifaya ni show inayosikika on Clouds FM Jumatatu mpaka Ijumaa kuanzia saa moja usiku kikiwa na mkusanyiko wa habari kumi kubwa za siku za siasa, muziki michezo na mengine.

#AMPLIFAYA May9 #10 Wasomali walalamikia kuonewa msako wa magaidi Kenya, Eastlegh High school Wanafunzi hawaendi wanaogopa kukamatwa ovyo.

#AMPLIFAYA May9 #9 Chama kipya cha kisiasa Tanzania ACT chasema ‘Samson Mwigamba Katibu Mkuu’

#AMPLIFAYA May9 #8 Mwanamke mmoja muuza Pombe haramu Kenya amekamatwa na polisi akiwa na kreti 57, imeua zaidi ya 86.

#AMPLIFAYA May9 #7 Kuanzia Jumatatu kila msafiri atakaguliwa kabla ya kupanda basi la Umma Nairobi na atapandia kituo maalum. #Ugaidi

#AMPLIFAYA May9 #6 Prezzo yuko Dar tayari kwa ajili ya show ya leo #MissIFM2014 #GoldenJubilee @AMB_Prezzo anasema hayuko mikono mitupu.

#AMPLIFAYA May9 #5 Edinson Cavani akataa kukubali kama atabaki PSG msimu ujao, za kuhamia Man United anasema hajui kama ni kweli au la.

#AMPLIFAYA May9 #4 David Kafulila: ‘Ushahidi wa kila kigogo alivyohusika kwenye ufisadi ninao, naomba mwongozo wako wa Spika nithibitishe’

#AMPLIFAYA May9 #3 Waziri Mkuu kuhusu UKAWA: ‘Tungekaa tuzungumze maana kama hoja ni matusi na kejeli tunaweza kukubaliana na tukarudi’

#AMPLIFAYA May9 #2 Jackline Wolper athibitisha alibadili dini na kupendana na Mwanaume ambae hawakuwa wamekutana, hakubadili sababu ya mali.

#AMPLIFAYA May9 #1 Mwanaume wa miaka 43 aliemuua mke wake Mwanza alimchoma visu zaidi ya 10 mbele ya watoto wake, wamesimulia wakilia.

Tupia Comments