Moja ya habari kubwa ambayo imekuwa gumzo ni pamoja na hii ya Mtu mmoja kufikishwa Mahakamani katika Wilaya ya Musoma, Mara kwa tuhuma zakuua watu 17 wa familia moja kwa kuwakata mapanga.
millardayo.com imezikusanya kutoka kwenye twitter yangu @millardayo stori zote kubwa kutoka katika Magazeti ya Tanzania leo July 31, 2017.
Familia 5 zenye wakazi zaidi ya 20 Msambweni, Tanga, zimekosa makazi baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi kuteketea kwa moto. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
Mtu mmoja amefikishwa Mahakamani, wilayani Musoma, Mara akituhumiwa kuua watu 17 wa familia moja kwa kuwakata na mapanga. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
TAKUKURU Tabora imemfikisha Mahakamani Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Itebulanda kwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
Mganga wa jadi wa Majomoto, Katavi amefikishwa Mahakamani kwa kukutwa na nyara za Serikali zenye thamani ya zaidi ya Tsh. 2.6m. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
Waziri Mkuu Majaliwa ameagiza kuimarishwa ulinzi katika mipaka yote akisema Tanzania siyo lango la kupitishia dawa za kulevya. #HabariLEO.
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
Balozi wa Mchezo wa Mpira wa Kikapu, @jokateM ametoa rai wazazi kuwaruhusu watoto wa kike kushiriki michezo ili kukuza vipaji. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
Madiwani Manispaa ya Shinyanga wamesusia kikao chao baada ya kukosekana taarifa za utendaji kazi 2016/17 kwa sekta mbalimbali. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru amemuagiza DC wa Buhigwe kuwaweka rumande kwa saa 48 madiwani wasiohudhuria mbio za mwenge. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Msajili, Prof. Lipumba amesisitiza kumtambua Maalim Seif kuwa ni Katibu Mkuu wa Chama hicho. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
Serikali inawashikilia kwa mahojiano raia 16 wa Lebanon, Pakistan na Somalia waliopita Airport kwa vibali vilivyotiliwa shaka. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe leo anatarajia kutoa maazimio ya Kamati Kuu ya Chama iliyokutana kwa siku mbili mfululizo. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
"Ukerewe mimba si za kuuliza, wazazi hushirikiana na watuhumiwa na kuyamaliza."' – DC Estomih Chang'ah. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
ACT Wazalendo imeshangazwa na Serikali kushindwa kutimiza ahadi ya kugawa bure pembejeo za kilimo kwa wakulima wa korosho. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
DC Ukerewe amesema hali ya usalama wilayani humo si shwari kutokana na viashiria vinavyoweza kusababisha maafa wakati wowote. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Singida inatarajia kujenga Hospitali ya kisasa kwa nguvu za wananchi na wadau wa maendeleo. #MTANZANIA.
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
Wabunge 8 wa Viti Maalumu waliovuliwa uanachama CUF wamefungua kesi Mahakamani kuzuia walioteuliwa kuziba nafasi zao wasiapishwe. #MWANANCHI
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
Baada ya uchunguzi wa maabara katika Hospitali ya Muhimbili, imebainika watoto mapacha walioungana wanatumia moyo na ini moja. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
Rais wa Zanzibar Dr. Shain amesema kunahitajika sekta imara ya Bank ili kufanikisha azma ya Tanzania ya uchumi wa viwanda. #MWANANCHI.
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
Baadhi ya wakazi wa bonde la Ziwa Rukwa, Rukwa wameacha kutumia vyandarua vilivyotolewa na Serikali wakidai vinasababisha kunguni. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
Tetemeko dogo la Ardhi lenye kipimo cha richa 5.3 lililotokea Karagwe, Kagera na kudumu kwa muda wa chini ya sek. 5 limezua hofu. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
Imeripotiwa watu 8 wamefariki katika matukio mbalimbali ikiwemo mauaji na kuzama kwenye maji yaliyotokea ndani ya siku 9, Tanga. #Nipashe.
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
Waziri Mkuu Majaliwa ameitaka Idara ya Uhamiaji wilayani Kyela, Mbeya kuimarisha ulinzi ktk mipaka yake kudhibiti wahamiaji haramu. #Nipashe
— millardayo (@millardayo) July 31, 2017
ULIPITWA? “Homa ya Ini inatibika” – Daktari kaeleza chanzo, dalili na matibabu yake…tazama kwenye VIDEO hii kwa kubonyeza PLAY!!!