Michezo

Afrika imepata pigo kwa kumpoteza staa wa soka Afrika Kusini

on

Dunia ya soka leo imepokea taarifa za kusikitisha kuhusiana na moja kati ya mwanafamilia wa michezo kupoteza maisha, leo kutokea Afrika Kusini zimeripotiwa taarifa za kifo cha mchezaji wa club ya Free State Stars ya Afrika Kusini Sinethemba Jantjie.

Sinethemba Jantjie mwenye umri wa miaka 30 umauti umemkuta akiwa anatarajia kujiunga na club ya Bidvest ya Afrika Kusini, taarifa za kifo cha Sinethemba Jantjie zimekuja ghafla leo asubuhi na kueleza kuwa amepata ajali ya gari iliyopelekea kifo chake.

Taarifa zaidi za maandalizi ya mazishi yake zitatolewa baada ya familia kukaa kikao, Sinethemba Jantjie alijiunga na Free State 2016 akitokea Mbombela United, uwezo wake ulizidi kuvutia zaidi 2017 club Kongwe Afrika Kusini ya Kaizer Chief kutaka kumsajili ila dili lilishindikana kwa kutofikia makubaliano.

Msimamo wa Samatta kuhusu hatma ya Kapombe katika mgao wa Taifa Stars

Soma na hizi

Tupia Comments