TANESCO inapita kipindi kigumu cha upungufu wa umeme unao sababishwa na Ukame na Matengenezo ya mitambo.
Jumla ya Megawati 300 – 350MW zimepungua katika uzalishaji kwa siku hizi za karibuni.
Vituo vilivyoaathiriwa na ukame ni Kihansi(17MW vs 180MW, 63 hauzalishwi), Pangani(10MW vs 68MW, 58 hauzalishwi), Mtera(175MW vs 180MW, 5 hauzalishwi), Nyumba ya Mungu(3MW vs 8MW, 5 hauzalishwi).
Vituo vilivyo kwenye Matengenezo Kidatu(150MW vs 200MW, 50 hauzalishwi), Ubungo III (32MW vs 112MW, 80 hauzalishwi), Kinyerezi II(195MW vs 248MW, 53 hauzalishwi).
Jumla ya umeme ambao hauzalishwi kwa sababu ya ukame na matengenezo ni 414MW, kwa tarehe 23.11.2022 asubuhi.
Hatua za muda mfupi ni kuharakisha matengenezo ya mitambo hii ambapo inatarajiwa 90MW zitapatikana kama ifuatavyo:
a. Mashine moja ya 40MW ya Ubungo III , kurudi tarehe 25.11.2022.
b. Mashine ya Kidatu 50MW kurudi 28.11.2022.
c. Mashine mbili za Ubungo III 40MW kurudi kabla ya mwisho wa Disemba.
d. Kupatikana mashine mpya ya Kinyerezi I 90MW kabla ya mwisho wa Disemba.
Hii kama ukarabati ukikamilika kama ulivyopangwa itatupatia 220MW kwenye uzalishaji na kupunguza kadhia hii ya umeme. Mipango ya muda wa kati ambayo itapatikana mwezi Februari ni mashine nyingine ya 90MW itaanza kuzalisha umeme na kufikisha jumla ya 310MW.
Kwa kipindi hiki mvua zikipatikana hali ya umeme itaimarika mapema zaidi Na kama hakutakuwa na hitilafu nyingine itakayo jitokeza.
Tanesco itatoa taarifa kila wiki kwa kukutana na waandishi wa habari na kila siku katika tovuti ya club house.