Habari za Mastaa

BET wamuomba msamaha Nicki Minaj

on

Baada ya tuzo za Grammy kumalizika Jumapili ya February 10,2019 Rapper Nicki Minaj na Young Money wametangaza rasmi kutoshiriki tuzo za BET na kutotumbuiza kwenye onyesho la BET Experience mwaka huu baada ya kutupiwa dongo lilotoka BET.

Kupitia mtandao wa twitter wa kituo cha televisheni cha BET nchini Marekani kilionekana kurusha dongo kwa Nicki Minaj baada ya Cardi B kuondoka na tuzo ya Album bora ya Hip Hop(Invasion of Privacy) katika tuzo za Grammy na kauli hiyo ilimfanya Nicki kuchukua maamuzi hayo ikiwa pamoja na Lil Wayne ambaye alitajwa kutumbuiza kwenye tuzo za BET June,2019.

“Wakati huu Nicki Minaj amevuta na wigi lake” >>>BET

“Young Money haitoshiriki tena katika onyesho la BET Experience wala tuzo” >>>Nicki Minaj 

Baada ya muda mfupi BET wameamua kumuomba msamaha Nicki Minaj kutokana na kauli yao walioitoa dhidi yake na kusema kuwa wanampenda na wamechukua hatua ya kuifuta tweet hiyo na wako tayari kwa lolote ili kuliweka tukio hilo sawa.

Rapper Nicki Minaj ameahidi kuongea kila kitu kuhusu kushindwa kwake kupata tuzo kupitia Radio yake ya Queen Radio na kusisitiza kuwa mashabiki wanatakiwa kujua ukweli na pia Nicki alimaliza kwa kuwapongeza wale wote walioshinda tuzo za Grammy.

 

MAJIBU YA MONALISA VIDEO YA KAJALA NA PAULA ‘KUNA UBAYA AKICHEZA NA MWANAE?’

Soma na hizi

Tupia Comments