Shirika la Afya (WHO) limesema takriban nusu ya maambukizi ya Virusi vya Corona yaliyorekodiwa duniani wiki iliyopita ni kutokea Nchini India.
WHO imesema India imerekodi 46% ya maambukizi ulimwenguni pamoja na 25% ya vifo vyote vilivyoripotiwa wiki iliyoisha. Katika saa 24 zilizopita, watu 3,780 katika Taifa hilo wamepoteza maisha.
Waziri Mkuu, Narendra Modi na Serikali yake wamekosolewa kwa kutochukua hatua za kudhibiti wimbi la pili la mlipuko huo mapema. Matamasha ya Dini na mikusanyiko ya kisiasa iliyovutia maelfu ya watu imetajwa kuchangia maambukizi.