Michezo

Liverpool imemuongezea Brendan mkataba.

on

Screen Shot 2014-05-27 at 12.42.41 AMNi kocha mwenye umri wa miaka 41 ambae alianza kazi ya kuwa kocha mwaka 2008 kwenye club ya Watford na kisha kuhamia Reading mwaka 2009, 2010 akaenda Swansea City kisha 2012 akajiunga na Liverpool.

Pamoja na kwamba kocha huyu ameongezewa muda wa mkataba kuifundisha club hii, haijawekwa wazi ni miaka mingapi imeongezwa na aliishia tu kusema amejisikia vizuri kwa kuaminiwa na kukabidhiwa timu kwenye ukurasa mwingine wa kuendelea kuinoa.

Club hii ilithibitisha kwa kusema imemuongezea mkataba mrefu Rodgers ambae ni baba wa watoto wawili huku wa kwanza aitwae Anton (21) ambae anaichezea Oldham Athletic ambapo mtoto wa mwisho ni wa kike anaitwa Misch.

Story hii na nyingine zote millardayo.com ipo tayari kukufikishia kwa wakati popote ulipo, kaa karibu yangu kwa kubonyeza >>>  Twitter Instagram facebook ili kupata kila kinachonifikiwa ikiwemo pichaz, video, stori na mengine yote ya hii dunia.

Tupia Comments