Waziri wa Madini Dr Dotto Biteko amewataka wachimbaji wadogo nchini kutoa fedha za CSR kwa jamii zinazozunguka migodi kwani ni takwa la kisheria na kuacha ukali pale wanapoambiwa kutia fedha hizo tofauti na wawekezaji wanaotoka nje ya nchi.
Akizunguma na vyombo vya habari wakati wa uzinduzi wa kongamano la uwekezaji katika sekta ya Marini lililofanyika jijini Dar es salaam waziri Dr Biteko amezitaoa Halmashauri zinapokea fedha za CSR kiwashikilisha jamii husika ili kupanga nini kifanywe ambacho kitaacha alama kwa siku nyingi tofauti na fedha hizo kutumiwa kwa kutoa semina au kununua nguo za shule.
kongamano hilo la madini na uwekezaji litawavutia zaidi watu 2000, kutoka zaidi ya nchi 25 ulimwenguni itakayo ambatana na mkutano wenye zaidi ya wazungumzaji 100 wenye zaidi ya vipindi 20 na pamoja maonesho makubwa ya teknolojia na uvumbuzi.
kongamano la mwaka huu litaweka mazingatio juu ya uwekezaji wa kimataifa uchimbaji wa madini miradi mipya ,ushirikiano,teknolojia na uwezeshaji bila kusahau sera za serikali juu ya mazingira ,jamii na utawala,mikakati ya maendeleo ya sekta ya madini,uchimbaji wa madini endelevu pamoja na uzalishaji wa ndani.