Mix

Maneno ya Quick Rocka baada ya kumsikia Luffa akimzungumzia Radioni

on

Kwenye Uherd leo July 10, 2017 mtangazaji Soudy Brown ameinasa hii ya Quick Rocka kudaiwa kutomlipa Producer wake wa zamani Luffa kwenye baadhi ya kazi alizofanya kabla hajaondoka na kutoshirikishwa wakati nyimbo hizo zinapotoka ukiwemo wimbo wa OMG.

Soudy amewatafuta Luffa na Quick Rocka:>>>”Ndio mara ya kwanza na sijui kwa nini. Tangu niondoke, project zangu wanatumia wanavyotaka wao. Mimi lazima wanipe taarifa lakini wanazingua kiukweli.” – Luffa.

Kwa upande wa Quick Rocka alipotafutwa alikuwa na haya ya kuyasema:>>>”Hayo malalmiko mbona mimi hajaniambia chochote? Kwa nini anakuja kulalamika kwenye media na anajua mimi nina ofisi, mbona hajakuja kunambia? Unajua kuna vitu vingine hutakiwi kuviongea. Mimi sitaki kuchafua chochote kuna vitu vingine tunaviacha kama vilivyo.” – Quick Rocka.

Bonyeza Play hapa chini kusikiliza Full story..

EXCLUSIVE: Staa wa BSS aeleza sababu za kuacha Bongofleva na kuimba Gospel

Soma na hizi

Tupia Comments