Mahakama ya Nigeria , inatarajiwa kutoa uamuzi wake hii leo kuhusu uchaguzi wa februali uliomuweka Rais Bola Tinubu Madarakani na ambao upinzani unapinga vikali.
Usalama unaonekana kuimarishwa nje ya mahama hiyo baada ya siku 180 kukamilika tangu mahakama ya rufaa kuliunda jopo maalum la majaji nchini Nigeria watakaosikiliza kesi hiyo.
Kulingana na chama cha upinzani nchini humo ni kwamba uchaguzi huo uliompa Rais Bola Tinubu ushindi ulikumbwa na udanganyifu mkubwa.
Serikali ya Tinubu imetupilia mbali madai yote na kuonekana kujiamini, na kuangazia uadilifu wa mahakama.
Malalamiko ya kupinga ushindi wa Bola Tinubu yaliwasilishwa mwezi Machi pamoja na wagombea kadhaa wa urais akiwemo kiongozi mkuu wa upinzani Atiku Abubakar aliyeshika nafasi ya pili na mtu wa nje Peter Obi aliyeshika nafasi ya tatu.
Haya yakijiri Rais Bola Tinubu ameeekea nchini India ili kuhudhuria mkutano wa mataifa tajiri duniani G20.
Tangu Nigeria irejee kwenye demokrasia mwaka 1999 miongo mitatu baada ya utawala wa kijeshi, uchaguzi umekuwa ukiishia mahakamani, ingawa hakuna pingamizi iliyowahi kutengua matokeo.