Habari za Mastaa

Picha 17 za Diamond hapa South Africa jinsi ilivyokua akirekodi kolabo na Mafikizolo June 9 2014

on

2

Hapa ni kwenye gari safari ya kuelekea studio ndio inaanza, Mameneja Bab Tale kushoto na Salam kulia pembeni na Diamond

Hatimae mpango wa Mafikizolo wa South Africa ambao ni mastaa wa hit single ya ‘khona’ waliochukua tuzo mbili kwenye MTV Africa music awards 2014 kufanya kolabo na Diamond umefanikiwa kwenye usiku wa June 9 2014.

Diamond pamoja na mameneja wake wawili ambao ni Salam na Bab Tale waliongozana mpaka kwenye studio za msanii mkongwe aitwae Oskido ili kurekodi kolabo hiyo ya Mafikizolo, kundi la Afrika kusini lililorudi kwenye chati kupitia mikono ya Oskido.

3

Ndio tunawasili kwa Oskido, mtu wako wa nguvu nilikuepo kuhakikisha kila kinachotokea kinakufikia

Kama hukusikiliza Clouds FM Top 20 Jumapili ya June 8 2014, wakati wa kufanya mazoezi ya tukio la MTV kwenye tuzo za Mama Durban South Africa June 7 2014, Mafikizolo waliomba kurekodi wimbo na Diamond baada ya kushawishika kufanya nae kolabo hivyo wakaahidi kushughulikia gharama zote za kumuongezea Diamond muda wa kuendelea kukaa South Africa pamoja na kubadili ticket ya ndege ili wakamilishe kazi yao.

4

9

Oskido ni msanii mkubwa sana na mwenye uwezo hapa South Africa na anapendwa sana ila pamoja na ukubwa wa jina lake, huwa hajiweki juu kabisa… ni mpole na simple kila wakati, nakumbuka hapa yeye ndio aliomba kupiga picha na Diamond.

8

Diamond alipoingia studio alikua bado hajapewa topic ya wimbo, yani alikua hajui wimbo unahusu nini ila dakika kadhaa baadae akaanza kushusha mistari yake… alipoingia kuingiza voco ya kwanza Mafikizolo pamoja na Producer wakampigia makofi na kusmile kuashiria kijana katishaa.

7Bado  jina la wimbo na tarehe ya kutoka havijajulikana ila kila kitu kikiwa tayari utakipata kupitia hapahapa millardayo.com

6

5

16

Mafikizolo na Diamond

15

14

Upande mwingine ambao wengi hawaujui, Diamond ni mtani na anachekesha sana, ana aina yake ya kuhadithia kitu mpaka ukacheka… ilikua goodtimes studio kiukweli

13

Hapa walikua wanacheza Theo wa Mafikizolo pamoja na Diamond.

12

11

10

21

Diamond anaipenda sana kazi yake, yani pamoja na Mafikizolo kuondoka studio baada ya kumaliza kurekodi… Diamond aliamua kubaki kuhakikisha roho yake imeridhika

20Ikitangaza kutoka hapa Johannesburg South Africa leo June 10 2014 kwenye AMPLIFAYA ya Clouds  FM kuanzia saa moja usiku utasikia stori za walivyokua studio pamoja na jinsi Mafikizolo walivyoanza kufahamu kuna mtu anaitwa Diamond Platnumz kutoka Tanzania East Africa.

Ili kupata kila kitu ungana na mimi nikutumie kila kinachonifikia kwa kubonyeza hapa na kuwa Mwanafamilia twitter instagram facebook

Video za ilivyokua studio wakati wakirekodi zitakuja on AyoTV so kaa karibu kwa kujiunga na AyoTV twitter kwa kubonyeza HAPA

Tupia Comments