Marekani imetangaza kuachana na ushirikiano wake wa kijeshi na nchi ya Rwanda kwa tuhuma za Kigali kuwatumia watoto kama wanajeshi na kuunga mkono waasi wa M23.
Kwa mjibu wa msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekeni, nchi ya Rwanda umeongezwa katika orodha ya mataifa 19 ambayo Marekani imesitisha ushirikiano wake wa kijeshi kutokana kupata ushahidi kuwa utawala wa nchi husika huwataumia watoto katika vikosi vyake au makundi yenye silaha ambayo serikali inaunga mkono.
Afisa huyo wa Marekani ni kwamba Rwanda imeongezwa katika orodha hiyo kutokana na jeshi lake la RDFkuunga mkono waasi wa M23 mashariki wa DRC ambao wamekuwa wakiteleza mauwaji ya raia na pia wamekuwa wakisajili watoto kuwa wapiganaji wake.
Mwaka 2013 Marekani pia ilisitisha msaada wake kwa jeshi la Rwanda kwa tuhuma sawia na hizi.
Hata hivyo Rwanda imendelea kukana madai ya kuunga mkono waasi wa M23, wakati huu reipoti ya umoja wa mataifa ikisema zaidi ya watoto 17,500, wameondolewa kwenye makundi ya waasi tangu mwaka 2017.
Rais wa DRC tayari amepongeza hatua hiyo ya Marekani kusitisha ushirikiano wakewa kijeshi na Rwanda.
Chanzo:RFI