Wizara ya Mambo ya Nje ya Algeria Jumatatu ilitoa taarifa ikisema Niger imekubali shauri la usuluhishi la Algeria kwa ajili ya kutafuta utatuzi wa kisiasa juu ya mgogoro unaoendelea sasa nchini Niger.
Taarifa hiyo ilisema baada ya Niger kukubali shauri la usuluhishi la Algeria, rais Abdelmadjid Tebboune wa Algeria amemwagiza waziri wa mambo ya nje aende Niamey, mji mkuu wa Niger, ili kuanza mazungumzo ya matayarisho na pande zote husika.
Waziri wa Mambo ya Nje na Diaspora wa Algeria Bw. Ahmed Attaf mwishoni mwa Agosti alisema, Algeria imependekeza utatuzi wa kisiasa ili kuisaidia nchi jirani ya Niger kutatua mgogoro unaoendelea.
Lengo kuu la utatuzi wa kisiasa ni kuweka muda wa miezi sita wa kuandaa na kutekeleza utatuzi wa kisiasa utakaohakikisha utawala wa kikatiba na kidemokrasia nchini Niger unarejeshwa.