Chama kikuu cha upinzani nchini Uganda nchini Uganda National Unity Platform (NUP) kimesema kiongozi wake Robert Kyagulanyi almaarufu Bobi Wine amekamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe alipokuwa akirejea kutoka nje ya nchi.
Chama cha (NUP) kilikuwa kikipanga kufanya mikutano na kuelezea kukamatwa kwake kama “mwoga”.
‘’Amechukuliwa akiwa bado kwenye ndege na kupelekwa katika maeneo yasiojulikana. Hadi muda huu hatujui yuko wapi,’’ Katibu Mkuu wa chama cha NUP David Lewis Rubongonya ameambia waandishi wa habari katika kituo cha ukaguzi wa kiusalama katika barabara kuu ya Entebbe Kampala ambapo alikuwa amezuiliwa kwenda uwanja wa ndege wa Entebbe kulingana na gazeti la Daily Monitor.
Kabla ya Bw Kyagulanyi kurejea, polisi walikuwa wamesema msafara uliopangwa kutoka uwanja wa ndege haukuwa halali.
Hata hivyo, Daily Monitor imeweka ujumbe kwenye mtandao wa X na kumuonyesha mbunge Mathias Mpuuga akiwa na Bobi Wine nyumbani kwake Magere, wilaya ya Wakiso muda mfupi baada ya kukamatwa uwanja wa Entebbe.