Kipa wa Manchester United Andre Onana anafikiria kuipa kisogo Cameroon kwenye kombe la mataifa ya Afrika mwezi Januari ili kuelekeza nguvu zake katika Manchester United.
Mkameroon huyo alihama kutoka Inter Milan kwenda Manchester United katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi.
Tangu kuhama kwake, amekuwa na shida kufikia matarajio yote na amekuwa chini ya shinikizo kutoka kwa mashabiki.
Sasa anafikiria kutupilia mbali Kombe la Mataifa ya Afrika mwezi Januari ili kusalia Old Trafford kulingana na ripoti.
Ripoti zimedokeza kuwa Onana huenda asijiunge na Cameroon kwa ajili ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwezi Januari.
Kipa huyo wa Man United anatazamia kurejesha kiwango chake cha ulinda mlango na anaweza kubaki na Mashetani Wekundu.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka Transfer News Live on X, “André Onana anasitasita kuchukua muda kutoka Manchester United ili kuichezea Cameroon kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika mwezi Januari baada ya kuanza maisha magumu Old Trafford.
Onana ameruhusu mabao 18 katika mechi tisa alizochezea Man United msimu huu huku akipambana kukidhi matarajio ya mashabiki.
Wakati huo huo, Man United nao wameanza vibaya msimu wa 2023/2024, wakiwa wamecheza mechi tisa, wamepoteza sita na kushinda tatu katika mashindano yote.
Timu ya Ten Hag itawakaribisha Brentford kwenye Uwanja wa Old Trafford siku ya Jumamosi wakijaribu kuepuka kichapo kingine msimu huu.