Huenda ukawa mmoja wa watu wanaoishi Tanzania lakini kuna vivutio vinavyopatikana Tanzania hujawahi kuvishuhudia na huwa unavisikia tu kama kuna vivutio vya namna hiyo.
Kama jibu ni Yes basi leo nakuunganisha kwenye safari moja ya Naibu Spika Dr. Tulia Ackson ambaye yupo kwenye ziara Mbeya na leo alikuwa na kazi moja tu kutembelea baadhi ya vivutio vya maajabu vilivyo kwenye mkoa huo.
millardayo.com ilikuwa sambamba na Naibu Spika kwenye kuyanasa matukio yote makubwa katika picha na hapa nimekusogezea kila kitu ikiwemo stori ya Daraja la Mungu iliyotolewa na Chifu wa Kabila la Wanyakyusa Lusajo Mwahesya:>>>”Daraja la Mungu ni daraja ambalo halijajengwa na mtu bali ni la asili toka kwa Mungu mwenyewe. Wagunduzi wa daraja hili ni Kabila la Wandali ambao walikuwa wakipita eneo hili na kutumbukia huku wakiwa wamejifunga mbuzi.
“Wananchi walikuwa wanahangaika kuvuka kutoka upande mmoja wa Mto kuelekea mwingine huku wengi wakiishia kupoteza maisha na baadae walimuomba sana Mungu ndio likagundulika hili daraja.” – Lusajo Mwahesya.
“Kwanza kabisa hili eneo zamani kabisa Wazungu walikuwa wakichimba na kusafirisha madini mbalimbali ambapo baadaye Mwalimu Nyerere alivyogundua kuwa wanafanya biashara ya kusafirisha madini yetu akaagiza waondoke ndani ya saa 24.” – Lusajo Mwahesya.
Safari ikaendelea hadi katika eneo linalofahamika kwa jina la Kijungu, Chief akaendelea kutupatia ufafanuzi kuhusu eneo hili pia:>>>”Kijungu ni neno la kilugha likimaanisha Chungu. Kuna daraja ambalo pia watu wanavuka lakini kwa masharti ya kupanda kwa kuanzia na mguu wa kulia kisha kushoto na wakati wa kurudi inakuwa kinyume chake na ukienda kinyume chake ni lazima utumbukie na kupoteza maisha.”
“Ikitokea mtu akadumbukia na kufariki kuna vitu huwa navifanya ndio naweza kuzama kwenda kutoa maiti hizo, kwa mwaka 2017 pekee nimetoa karibu maiti tisa za watu waliofariki kwenye mfereji huu.” – Lusajo Mwahesya.
Baadaye safari ikaendelea hadi katika maporomoko ya maji ya Kaporogwe ambapo Adam Kajera akatoa historia fupi:>>>”Kaporogwe ni maporomoko ya maji ambapo wazee wa zamani wanasema palikuwa panaitwa KUNDURIRO na jina la Kaporogwe lilianzia baada ya mzee aliyekuwa anachunga ng’ombe kisha fimbo yake ikamponyoka wakati anaifuata fimbo yake bahati mbaya akaja kudondokea huku. Kwa kuwa alikuwa anaitwa Kaporogwe basi watu wakaamua eneo hili kuitwa jina la huyo mzee ambaye kwa sasa nasikia anaishi Morogoro.”
VIDEO: Maamuzi ya Dr. Tulia baada ya kukuta ubovu kwenye shule aliyosoma Mbeya