Habari za Mastaa

DC Jokate atangaza kuleta mtihani mmoja wa shule za Secondary Kisarawe

on

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo amesema kwa Mwaka huu Kisarawe italeta mtihani mmoja wa Mock ya kwanza utakao wahusisha kidato cha nne katika shule zote za secondary wilayani humo, utakaoitwa Tokomeza Ziro Kisarawe form 4 Mock examination.

Jokate amesema hayo kupitia ukurasa wake kwa kuandika Post inayomuonesha akiwa na mwanamchi wake kutoka kijiji cha msanga aliyekuwa anamsahauri kurudia kufanya harambee ya kusaidia elimu baada ya kuona matokeo mazuri ya ufaulu mzuri wa wanafunzi Wilayani humo.

Jokate ameandika Haya… >>>>>“Mwaka huu tunafanya kwa mara ya kwanza kabisa pamoja na kambi tulizozoea, tokomeza zero Kisarawe form IV Mock Exams, mtihani moja Wilaya nzima na tayari tumeanza maandalizi hakuna kulala wala kukata tamaa mpaka kieleweke. Hii kampeni ni yetu sote” – DC Jokate Mwegelo

 

Soma na hizi

Tupia Comments