Michezo

Ronaldo kwa mara ya kwanza anaiaga Champions League robo fainali toka 2010

on

Usiku wa April 16 2019 ilichezwa michezo ya marudiano ya robo fainali ya UEFA Champions League kati ya FC Barcelona dhidi ya Man United katika uwanja wa Nou Camp na Juventus dhidi ya Ajax katika uwanja wa Allianz mjini Turin, bahati mbaya mashabiki wa Juventus wamepata pigo kwa timu yao kutolewa na Man United pia imetolewa.

Cristiano Ronaldo anaingia katika rekodi mbaya na ndio kwa mara ya kwanza msimu huu anaingia katika rekodi mbaya kwa timu yake anayoichezea kushindwa kufika robo fainali ya UEFA Champions League toka 2010, kufuatia kipigo cha magoli 2-1 (agg 3-2) kutoka Ajax, mgoli yakifungwa na Ronaldo dakika ya 28 kwa upande wa Juventus na Ajax yamefungwa na  Van De Beek dakika ya 34 na Matthijs dakika ya 67.

Baada ya vipigo hivyo kwa Juventus na Man United sasa wababe FC Barcelona na Ajax wanasubiri game za pili robo fainali kati ya Liverpool dhidi ya FC Porto na Man City dhidi ya Tottenham Hotspurs game ikitarajiwa kuchezwa katika uwanja wa Etihad.

Mwana FA kakutana na Jose Mourinho uso kwa uso, kamwambia yale maneno yake?

Soma na hizi

Tupia Comments