Mix

PICHA 8: Hali ilivyo Mwanza baada ya TRA kuvifungia zaidi ya vituo 10 vya mafuta

on

Mamlaka ya Mapato Tanzania ‘TRA’ imeendelea na oparesheni yake ya kukagua vituo vya mafuta na kuangalia kama vinafuata sheria na taratibu za kutumia mashine za kutolea risiti za kielektroniki maarufu kama EFPP zilizofungwa moja kwa moja kwenye pampu.

Unaambiwa oparesheni hiyo ni nchi nzima ambapo tayari Mwanza imeshuhudia vituo zaidi ya 10 vikifungiwa na TRA kutokana na kutofuata sheria wakati wa kutoa risiti huku kutoka mjini hadi Buhongwa ni vituo vitatu pekee ndio vinafanya kazi.

millardayo.com imekuwa ikitembelea kwenye vituo hivyo na kufanikiwa kuzinasa picha 8 zikionesha hali ilivyo baada ya baadhi yake kufungwa na TRA.

VIDEO: Walichokizungumza Star TV baada ya kufungiwa na TRA!!!!

Soma na hizi

Tupia Comments