Baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kuvamia ofisi za Clouds TV na kuwalazimisha watangaza wa kipindi cha Shilawadu kurusha kipindi kinachomuhusu Askofu Gwajima kikiwa hakijamaliziwa maandalizi kinyume na taaluma ya habari, Leo March 22, 2017 Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limefanya kikao cha maamuzi dhidi suala hilo.
TEF pamoja na Club ya Waaandishi wa Habari Dar es saalam (DCPC) na Umoja wa Club za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC) zimepitisha maamuzi matatu ikiwemo.
- Kulaani vikali vitendo vya RC Paul Makonda
- Kutoandika na kutangaza habari zozote kuhusu Paul Makonda kwenye chombo chochote cha Habari.
- Kumtangaza RC Makonda kama adui wa Uhuru wa Vyombo vya Habari pamoja na yeyote atakayeshirikiana naye.
Unaweza kusoma kila kitu kwenye tamko hili hapa chini.
Jukwaa la Wahariri TEF, Club ya Wanahabari DSM (DCPC) na Umoja wa Wanahabari Tanzania UTPC zimekubaliana kutoandika habari za RC Makonda. pic.twitter.com/wPwBeO5T3o
— millardayo (@millardayo) March 22, 2017
VIDEO: Ulipitwa na kauli ya Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC kuhusu Rais Magufuli na RC Makonda? Bonyeza hapa kutazama