Michezo

Imenifikia TOP 5 ya wachezaji soka wenye majina marefu zaidi duniani …

on

Najua mtu wangu imekuwa ni kawaida kusikia majina ya wachezaji pindi wanapotangazwa kupitia Television au Radio wakati mpira ukichezwa, wengi huwa tunatambua majina ya kawaida na mafupi kutokana na namna ya matamshi ambayo mtangazaji hutamka. Stori kutoka thebesteleven.com hii ndio Top 5 ya majina marefu zaidi kwa wachezaji soka, huenda wakawepo wengine ila imenifikia list hii mtu wangu.

Manuel Marouan da Costa Trindade Senoussi, ni staa aliyezaliwa Saint Max Ufaransa ambaye jina lake lina jumla ya herufi 36. Kwa sasa anaitumikia klabu ya Olympiacos inayoshiriki Super League ya Ugiriki, amewahi pia kuichezea West Ham United ya Uingereza, staa huyu huwa anacheza kama beki wa kati.

orig

Manuel Marouan da Costa Trindade Senoussi

Henrique Hilário Meireles Alves Sampaio, ni mzaliwa kutoka Ureno ambaye amestaafu kucheza soka, alicheza katika nafasi ya Golikipa, amebahatika kucheza kwenye timu yake ya taifa na klabu tofauti ikiwemo Chelsea ya Uingereza. Jina lake lina jumla ya herufi 35.

hilario_chelsea145254ba_664x373

Henrique Hilário Meireles Alves Sampaio

Fredrik Olof Esaias Stoor Siekkinen, anajulikana zaidi kama Fredrick Stoor ambaye amezaliwa Sweden, kwa sasa anaichezea timu ya Viborg FF inayoshiriki Danish Superliga ya Denmark. Stoor anacheza kama beki wa kulia. Ameshawahi kuitumikia klabu ya Fulham ya Uingereza pamoja Derby Country na timu ya taifa ya Sweden. Jina lake lina herufi 31.

fredrik-olof-esaias-stoor-siekkinen_1nvsf5h930hax1khdljttb3fvg

Fredrik Olof Esaias Stoor Siekkinen

Geovanni Deiberson Maurício Gómez,  ni Mbrazil ambaye tayari amestaafu kucheza soka, anatambulika zaidi kwa jina la Geovanni, alikuwa akicheza kama kiungo mshambuliaji akiwa na uwezo wa kucheza pia nafasi ya winga. Geovanni amewahi kuzichezea FC Barcelona, Manchester City, Hull City, Benfica na timu ya taifa ya Brazil. Jina lake lina jumla ya herufi 30.

Geovanni1

Geovanni Deiberson Maurício Gómez

Diniyar Rinatovich Bilyaletdinov ni jina ambalo limekuwa likitumika na wengi kumuita, ni mzaliwa kutoka Moscow, Urusi ambaye hivi sasa anaitumikia timu ya Rubin Kazan inayoshiriki Ligi Kuu Urusi. Bilyaletdinov amewahi kucheza katika nafasi ya kiungo akiwa na vilabu vya Locomotive Moscow, Everton na amecheza timu ya taifa ya Urusi. Jina lake lina herufi 30.

44246001_bilyaletdinov_afp416

Diniyar Rinatovich Bilyaletdinov

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments