Kipa wa zamani wa Manchester United David De Gea yuko tayari kujiunga na Newcastle United kama mbadala wa Nick Pope, chanzo kiliiambia shirika la habari la ESPN.
Pope aliteguka bega wakati wa kipindi cha pili cha ushindi wa 1-0 wa Newcastle dhidi ya United siku ya Jumamosi.
Kipa huyo wa England anaweza kuondolewa kwa hadi miezi mitano,uwanjani.
De Gea amekuwa hana klabu tangu alipoondoka United mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kumalizika kwa mkataba wake.
Mhispania huyo alikaa Old Trafford kwa miaka 12 akicheza mechi 545,alikuwa sehemu ya timu iliyoshinda taji mnamo 2012-13 na alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa kilabu mara nne.
Nafasi yake ilichukuliwa na mchezaji wa kimataifa wa Cameroon André Onana, ambaye amekuwa na mwanzo mgumu katika maisha yake ya soka United. Onana, aliyesajiliwa kwa pauni milioni 43 ($54m) kutoka Inter Milan msimu wa joto, alikuwa na makosa kwa mabao mawili katika sare ya 3-3 dhidi ya Galatasaray ambayo yameifanya timu ya Erik ten Hag kukabiliwa na kuondolewa kwenye Ligi ya Mabingwa.
De Gea amekaa Manchester kwa muda tangu aondoke United na alipigwa picha akiwa na umati wa watu kwenye mchezo wa wanawake kwenye Uwanja wa Leigh Sports Village mwezi Oktoba.
Chanzo kimoja kiliiambia ESPN kwamba amekuwa akifanya mazoezi mara kwa mara na atakuwa tayari kukubali ofa ikiwa anahisi ni hatua sahihi.