Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema serikali haita wavumilia wakandarasi wanaosuasua katika utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini (REA) na hivyo kupelekea adha kwa mwananchi kukosa huduma hiyo ili hali Serikali imetoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo.
Naibu waziri Kapinga ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha sharaka kata ya makuyuni wilayani korogwe mkoani Tanga mahali ambapo kunatekelezwa mradi wa umeme vijiji wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 150 ambao umeshindwa kukamilika kwa wakati kutokana na kusua kwa mkandarasi.
“Huyu ni mkandarasi msumbufu sana na tutaangalia hata mbeleni tusimpe kazi tena hata kama ameomba radhi miaka yote miwili anapambana na kilomita moja hata tukimpa kazi nyingine ataweza kweli? hatuta wavumilia wakandarasi wabovu”
“mkandarasi amekuwa na sababu nyingi sana katika kutekeleza mradi huu wakati wote anataja changamoto sijui mvua sijui barabara mbovu kwani miaka yote hiyo miwili hakufahamu changamoto hizo kwakweli wananchi wanataka umeme nasio maneno”
wakala wa nishati (REA) inatekeleza miradi minne wilayani korogwe ikiwemo mradi huo wa sharaka ambapo utanufaisha vijiji 27 na unatarajia kutumia shilingi milion 150 mpaka kukamilika kwake.