Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, HESLB imetoa taarifa yake juu ya hali ya urejeshaji wa Mikopo ya Wanafunzi walionufaika na mikopo hiyo ambapo imesema kiasi cha Tsh. Bilioni 13.7 kimerejeshwa kutoka kwa mnufaika mmoja mmoja.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru amesema:>>>”Mpaka sasa Serikali imewekeza takribani Trilioni 2.5 katika kulipia Wanafunzi ambao wanasoma na imelipia Wanafunzi wapatao karibu 380,000 tangu shughuli za kukopesha zilipoanza.
“…mpaka tunamaliza mwaka tulikuwa tumekusanya bilioni 116 kwa mwaka huu wa 2016/17 – mwaka ulioanza July mwaka jana mpaka tulipofikia hapa. Tunawapongeza sana wale walioweza kufanikisha lengo hili.” – Abdul-Razaq Badru.
EXCLUSIVE: Majibu ya Tundu Lissu kuhusu kumfuta uanachana Waziri Mwakyembe!!!