Habari za Mastaa

50 Cent kwenye headlines tena, anataka kuwa ‘baba mwenye nyumba’? Ishu ni hii…

on

50 cent

Msanii wa hip hop Marekani 50 Cent amekuwa akiingia kwenye headlines mbalimbali mara baada ya kutangaza kuwa amefilisika.

Headlines juu yake zinazidi kukua kila siku na safari hii headlines zinazomhusu 50 Cent ni za yeye kutafuta mpangaji wa nyumba yake iliyopo Connecticut Marekani.

GHETTO LA 50

Taarifa hizi zilianza kusambaa kwa fujo siku ya jumatano baada ya kukamilisha mkutano wake na Wanasheria.

Mwanasheria wa 50 Cent, Stephen Savva alisema japo hakuna mkataba wa upangishaji uliofikiwa kupangisha nyumba yake ya Farmington Mansion ambayo 50 aliinunua mwaka 2003…wamekuwa wakifanya mipango ya kupangisha nusu ya nyumba hio yenye vyumba 21, majiko 9 na casino lakini mpaka sasa rapper huyo hajabahatika kupata mpangaji.

50cent2

Bado hatujasikia kiasi cha pesa ambacho msanii huyo atatoza kama kodi ya nyumba, ila documents zilizowasilishwa Mahakamani zinasema kuwa 50 Cent amekuwa akilipa dola 72,000 (Tzs.Milioni 144) kwa mwezi tu kama hela ya matunzo ya nyumba hiyo ambayo ni tofauti na kodi yake ya nyumba!

Duh! Unadhani hapa 50 Cent atapata mpangaji kweli kama matunzo yenyewe ndio hayo?

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments