Habari za Mastaa

50 Cent kafikishwa Mahakamani na anadaiwa faini, ni kweli amefilisika??

on

fif

Kumekuwa na stori nyingi kuhusiana na rapper 50 Cent kutoka Marekani, moja kubwa kuhusu yeye ilikuwa ni stori inayohusiana na yeye kuvijisha video ya ngono ya mwanadada Lastonia Leviston ili kumuaibisha mshindani wake kwenye muziki, Rick Ross.

Kesi ikaenda Mahakamani na hukumu inaonesha 50 Cent anatakiwa alipe faini ya dola Mil.5 sawa na Billioni 10 za Kitanzania kwa mwanadada huyo.

NEW YORK, NY - JUNE 02:  Curtis "50 Cent" Jackson visits "Extra" in Times Square on June 2, 2014 in New York City.  (Photo by D Dipasupil/Getty Images for Extra)

Headlines za 50 Cent leo ziko tofauti, Mwanasheria wa rapper huyo ametangaza kwamba jamaa kafilisika, Mahakamani zimepelekwa document zinazoonesha kuwa 50 Cent ana madeni yasiyopungua dola Mil.50 sawa na Bil.100 za Kitanzania.

2011 Consumer Electronics Show Showcases Latest Technology Innovations

Sheria inatoa nafasi kwa mtu kupeleka Mahakamani documents na vielelezo vingine vinavyompa nafasi kujilinda na kuokoa baadhi ya biashara zake wakiwa wanakabiliana na madeni makubwa.

Msemaji wa mwanasheria wa 50 Cent, Travis Carter amesema msanii huyo amelazimika kufanya hivyo kuweka mambo yake ya kiuchumi sawa lakini hii haimanishi rapper huyo hana uwezo wa kusimamia biashara ama pesa zake.

DAYTONA BEACH, FL - FEBRUARY 22:  Curtis "50 Cent" Jackson stands in Victory Lane prior to practice for the NASCAR Sprint Cup Series Daytona 500 at Daytona International Speedway on February 22, 2014 in Daytona Beach, Florida.  (Photo by Jared C. Tilton/Getty Images)

Kwenye Interview moja 50 Cent alisema: “Kufanya hivi kunanilinda mimi na maslahi yangu ya biashara nyingi ninazojihusisha nazo, ni kawaida kwa wafanyabiashara kufanya hivi ni sawa na kulinda mifuko yangu. Uwezo ninao sema narekebisha tu vitu fulani kwa faida yangu na wadeni wangu”>>> 50 Cent.

<> at Marquee Nightclub In The Cosmopolitan on January 7, 2011 in Las Vegas, Nevada.

Travis Carter alisema: “Maslahi yake ya kibiashara yataendelea kama kawaida na ataendelea kujihusisha na biashara zake nyingine na kuendelea kufanya kazi kama entertainer”.

50-cent1

Kwa sasa rapper 50 Cent anaishi Connecticut Estate kwenye nyumba aliyoinunua kutoka kwa bondia wa zamani, Mike Tyson mwaka 2003.

 Unahitaji chochote nachokipata kikufikie? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Soma na hizi

Tupia Comments