Amplifaya Top10

Stori 10 za AMPLIFAYA June 26 2014

on

Radio studio 1Amplifaya ni show inayosikika Jumatatu mpaka Ijumaa kupitia CloudsFM kuanzia saa moja usiku mpaka saa tatu ikiwa na mkusanyiko wa stori kumi kubwa za siku za siasa, muziki, michezo na mengine.

#AMPLIFAYA #June262014 #10 Vifo elfu 35 vya saratani kwa mwaka Tanzania vinachangiwa pia na mafuta ya kula yanayokaa juani sana #Bungeni

#AMPLIFAYA #June262014 #9 Ni watanzania 113 wamefungwa gerezani nchini Brazil kutokana na kesi za dawa za kulevya.

#AMPLIFAYA #June262014 #8 Imegundulika pia katika aina 19 za Shisha zilizopigwa marufuku Kenya, zimechanganywa na Cocaine na kuberi.

#AMPLIFAYA #June262014 #7 Miongoni mwa Shisha 19 zilizopigwa marufuku Kenya ni pamoja na Nakhala Molasses Tobacco Apple na Formulated Shisha.

#AMPLIFAYA #June262014 #6 Sophia Simba: ‘Ukeketaji umekithiri Manyara 71%, Dodoma 64% na Singida 51%.. Dar na Pwani wameanza kukeketa pia’

#AMPLIFAYA #June262014 #5 Suarez aadhibiwa kutocheza kwa miezi minne kutokana na kumng’ata Giorgio Chiellini kwenye World Cup.

#AMPLIFAYA #June262014 #4 Wachezaji timu ya taifa Ghana Sulley Muntari na Kevin Boateng wamefukuzwa kwenye timu hiyo kwa ukosefu wa nidhamu.

#AMPLIFAYA #June262014 #3 Uhuru wa Kenya ndio Rais anayejishughulisha zaidi kwenye Twitter barani Afrika, kampiku Kagame. -BBC

#AMPLIFAYA #June262014 #2 John Mnyika: ‘Kama msemaji wa CHADEMA, natoa wito kwa msajili wa vyama vya siasa aweke wazi ripoti za vyama vyote vya siasa’

#AMPLIFAYA #June262014 #1 CHADEMA kuhusu walioandamana jana >> ‘wengine wamefukuzwa muda mrefu, wengi wao sio hata Wajumbe wala Wanachama’

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta FB

Tupia Comments