Stori Kubwa

Watu wangu mnaopenda kuvuta Shisha, hizi zimepigwa marufuku Kenya

on

SHISHA 12Imekua ni kawaida sasa hivi kwenda kwenye sehemu mbalimbali za starehe na kukutana na huduma ya uvutaji wa Shisha (sheesha) ambayo hutolewa kwa malipo.

Pamoja na kwamba wengi wameamini haina madhara, huko Kenya madhara yameonekana baada ya aina 19 za ladha za Shisha kugundulika kuwa zimechanganywa na dawa za kulevya ikiwemo Cocaine, Heroine, bangi na kuberi.

Baada ya utafiti shirika la kupambana na mihadarati na dawa za kulevya nchini Kenya ndio limepiga marufuku utumiaji wa aina hizi za shisha ambapo yeyote atakaepatikana akiuza au kutumia aina hizo atafikishwa Mahakamani.

Kwa taarifa zaidi unaweza kubonyeza play kusikiliza sauti ya Citizen TV Kenya ambayo iko mwishoni chini kwenye hii post.

SH 1

Baadhi ya Shisha zilizopigwa marufuku.

SH 2

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta FB

Tupia Comments