Tume ya Mipango nchini imesema hadi sasa zaidi ya wananchi laki sita na na kaya zaidi elfu kumi zimesha toa maoni ya muelekeo wa Dira ya maendeleo ya mwaka 2050 huku rasimu ya Kwanza ya dira ya maendeleo ikitegemewa kukamilika novemba mwaka huu.
Akizungumza juu ya kongamano la kitaifa la utoaji maoni litakalo fanyika chuo kikuu cha Dar es salaam tarehe 8 ya mwezi huu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango ya TaifaLawrence Mafuru amesema kongamano hilo litakalo ongozwa na Makamu wa Rais wa TanzaniaDr Philip Mpango litakuwa ni sehemu ya uchukuaji maoni ya wananchi juu ya uundaji dira mpya ya maendeleo itakayo beba na kujibu maswali ya wananchi.
Kuhusu mchakato wa uchukuaji maoni na juu ya kukamilika kwa rasimu Mafuru amesema kasi inayo kwenda nayo tume hiyo kwa sasa ni ya kuridhisha ambapo kati ya kaya elfu saba zilizolengwa kufikiwa katika kutoa maoni kaya zaidi ya elfu kumi zimefikiwa huku kati ya watu milioni moja tayari watu laki sita wamefikiwa na bado mchakato unaendelea .
Tume hiyo iliundwa na Rais wa Tanzania ili kuandaa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya mwaka 2050 baada ya dira ya sasa kuelekea mwisho mwaka 2025 ambapo Mwenyekiti wa Tume huyo ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania