Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un alimpa Rais wa Urusi Vladimir Putin mbwa[ 2]aina ya Pungsan, jamii ya kienyeji, vyombo vya habari vya serikali KCNA viliripoti Alhamisi.
Kim na Putin walionekana wakiwatazama mbwa hao waliokuwa wamefungwa kwenye uzio , wakati wa sehemu iliyorushwa na Televisheni Kuu ya Korea inayodhibitiwa na serikali siku ya Alhamisi.
Pia waliendesha kwa zamu kila mmoja gari la abiria aina ya Aurus lililojengwa na Urusi siku ya Jumatano.
Rais wa Urusi Vladimir Putin na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un walitia saini makubaliano Jumatano ambayo yanaahidi kusaidiana ikiwa nchi yoyote inakabiliwa na “uchokozi,” mkataba wa kimkakati ambao unakuja wakati wote wawili wakikabiliana na mizozo inayoongezeka na Magharibi.
Maelezo ya mpango huo hayakufahamika mara moja, lakini inaweza kuashiria uhusiano mkubwa kati ya Moscow na Pyongyang tangu kumalizika kwa Vita Baridi.
Viongozi wote wawili walielezea kama uboreshaji mkubwa wa uhusiano wao, unaojumuisha usalama, biashara, uwekezaji, uhusiano wa kitamaduni na kibinadamu.
Mkutano huo ulikuja wakati Putin alipoitembelea Korea Kaskazini kwa mara ya kwanza baada ya miaka 24 na Marekani na washirika wake walieleza wasiwasi wao juu ya uwezekano wa mpango wa silaha ambapo Pyongyang itaipatia Moscow silaha zinazohitajika sana kwa ajili ya vita vyake vya Ukraine, badala ya misaada ya kiuchumi na uhamisho wa teknolojia ambao unaweza kuongeza tishio linaloletwa na mpango wa silaha za nyuklia na makombora ya Kim.
.